Baada ya Polisi nchini Kenya kuvamia nyumba ya mtoto wa Rais Mstaafu, Jomo Uhuru Kenyatta, Baba yake Uhuru amezungumzia kisa hicho akisema kulikuwa na mpango wa kumwekea Silaha na dawa za kulevya wakati wa operesheni ya Ijumaa Julai 21, 2023.
Akizungumzia suala hilo mbele ya waandishi wa Habari, Uhuru amesema jambo hilo la Bunduki limezingirwa na propaganda nyingi, ili kugeuza mawazo kutoka kwa kile ambacho kimekuwa kikitokea na kwamba anaamini walitaka kupanda dawa na silaha katika boma la mwanaye.
“Tukio hili limeniumiza sana nilienda kwa sababu ya simu ya dhiki kutoka kwa mwanangu sikuwa mlevi, niliumia sana ila ni kweli wanangu wawili wanamiliki bunduki sita kwa jumla, tatu kila mmoja, na bunduki zote zimesajiliwa kisheria,” alifafanua Kenyatta.
Aidha, meongeza kuwa bintiye Ngina Uhuru hamiliki Bunduki na hakuna hata mmoja wa watoto wake ambaye amepokea amri ya kusalimisha silaha zake kama inavyodaiwa kwenye vyombo vya Habari na tayari Serikali ilithibitisha kuvamia nyumba tatu katika eneo la Karen jijini Nairobi ili kutafuta bunduki 23 zinazodaiwa kutumika wakati wa maandamano ya kuipinga Serikali.
Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Kithure Kindiki alisema vyombo vya usalama vimepewa jukumu la kupekua eneo hilo kama sehemu ya operesheni pana inayolenga kuwaondoa watu walio na silaha za kiraia na viongozi wa magenge ya uhalifu yanayojulikana.