Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameziagiza Mamlaka zinazohusika na ujenzi wa masoko unaoendelea kwenye maeneo mbalimbali nchini wazingatie na waandae miundombinu kwa ajili ya wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga.

Majaliwa ameyasema hayo leo Januari 28, katika kikao na Viongozi wa Wamachinga Tanzania katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),   jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao hicho Waziri Mkuu amesema Wamachinga ni kundi muhimu katika kukuza pato la Taifa na takwimu za Wizara ya Viwanda na Biashara zinaonesha kuwa Sekta ya Viwanda Vidogo na Biashara Ndogo imetengeneza ajira, kukuza uchumi na kuondoa umasikini.

Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wamachinga wote nchini ikiwa ni pamoja na kuwapatia vitambulisho maalum vinavyowapa uhalali wa kufanya biashara zao bila bugudha.

Sekta hiyo ina jumla ya wajasiriamali milioni 3.1 ambao wameajiriwa ikiwa ni asilimia 23.4 ya nguvu kazi ya Taifa na imechangia asilimia 27 katika pato la Taifa.

Mostafa Mohamed kutimkia Galatasaray
Wataalam WHO watoka karantini