Watu watu wawili wameuawa kwa risasi na wengine saba kujeruhiwa vibaya katika jimbo la Louisiana nchini Marekani baada ya kushambuliwa kwa risasi na mtu aliyevamia jumba la sinema, jana usiku.

CNN imeripoti kuwa mshambuliaji huyo mzungu mwenye umri wa miaka 58 aliingia katika jumba la Sinema ikiwa ni dakika 20 tu baada ya sinema ya “Trainwreck” kuanza kutazamwa kisha akaanza kuwafyatulia risasi watazamaji hao.

Polisi wamesema kuwa mshambuliaji alijipiga risasi na kupoteza maisha baada ya kutekeleza tukio hilo. Wanausalama hao wameeleza kuwa tayari wameshatambua jina la mshambuliaji lakini hawako tayari kulitoa kwa kuwa bado uchunguzi wa tukio hilo unaendelea.

Tukio hilo limetokea muda mchache baada ya Rais Obama kuzungumzia udhibiti wa silaha nchini mwake kufuatia tukio baya la mauaji kwenye shule moja inayojulikana kwa jina la ‘Sandy Hook School’ mwaka 2012.

Hata hivyo, ombi la sheria ya kubana umiliki na matumizi ya silaha linapingwa na bunge la Congress.

Wema Sepetu Azua Mtafaruku Viti Maalum, Mwenyekiti UWT Atishia Kuhama CCM
Wagombea CCM Wapigana Ngumi