Wanaharakati pamoja na Muungano wa haki na Uhuru wa raia nchini Marekani, (ACLU) katika jimbo la Arkansas nchini Marekani wamepinga ujenzi wa jiwe moja kubwa lenye maandishi ya amri kumi (10) za Mungu, kwenye uwanja wa makao makuu ya bunge la jimbo hilo.
Ambapo, Muungano wa haki na uhuru wa raia nchini Marekani (ACLU), umeamua kupeleka kesi mahakamani na kutaka mnara huo wenye amri kumi za Mungu kuondolewa mara moja kwa madai ya kuwa unaleta mgawanyiko na unakiuka ahadi ya uhuru wa kidini kwa wote katika katiba ya Marekani.
-
Odinga apiga marufuku ngono siku ya uchaguzi
-
Marekani yaapa kula sahani moja na wahalifu wa mitandaoni
Uamuzi wa ujenzi wa mnara wa amri kumi za Mungu wenye urefu wa futi sita katika jimbo la Little Rock ulitolewa na wanasiasa mnamo mwaka 2015.
Seneta wa chama tawala cha Republican, Jayson Rapert, ambaye alikuwa katika mstari wa mbele wa kutaka kuwekwa kwa jiwe hilo amesema kuwa hatua hiyo inaenda sambamba na msimamo wa mahakama kuu ya Marekani, na hivyo ni jambo zuri kwa jimbo la Arkansas.