Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amewataka Wamiliki wa Makao ya watoto kuhakikisha wanatoa huduma kwa mujibu wa sheria na kanuni na kuhakikisha rasilimali zinazopatikana kwa ajili ya kuwasaidia watoto zinatumika kikamilifu.

Dkt. Gwajima ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa Wamiliki wa Makao ya Watoto Mkoa wa Dar es Salaam na kudai kuwa pamoja na makao mengi kufanya kazi nzuri na kwa uwazi, baadhi yamekuwa yakikusanya rasilimali na kujinufaisha wao zaidi kuliko walengwa.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima.

Amesema, pia baadhi ya wamiliki wa makao hayo wamekuwawakiwazuia na kuwapa vitisho Maafisa Ustawi wa Jamii  wanapofika kwenye makao hayo kufanya ufuatiliaji na ukaguzi wa utoaji wa huduma.

“Jambo hilo ni kosa kisheria kwa mujibu wa Kifungu cha 146 (2) (c) na adhabu yake ni kifungo kisichopungua mwaka mmoja au faini isiyopungua milioni 2 na isiyozidi milioni 10 au vyote viwili na pia ofisi ya msajili inaweza kufuta leseni ya kumiliki makao,”  amesema Dkt. Gwajima.

Chelsea imekwama tena, kujipanga upya
Kamwe: Tunakwenda Tanga kuchukuwa Ngao