Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki Jinai, Balozi Ombeni Sefue alisema, wakati wakizunguka kupata maoni ya Wananchi walikuwa wakiulizwa katika baadhi ya maeneo kuwa Tanzania ina Serikali ngapi, wakihoji uwepo wa uwingi wa majeshi.

Balozi Sefue ameyasema hayo hii leo Julai 20, 2023 katika Kikao cha Wajumbe wa Tume ya haki jinai, DPC na Wahariri wa Vyombo vya Habari Ikulu jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa hali hiyuo inaonesha Wananchi wana mkanganyiko juu ya suala hilo.

“Wakasema ‘mimi najua kila Serikali ina Jeshi moja sasa hapa ukiamka asubuhi hujui utakamatwa na Jeshi lipi?, utakamatwa na Polisi, TAKUKURU, Watu wa misitu na wanyamapori, kwahiyo hiyo ndio dhana ya Wananchi,” alisimulia Balozi Sefue.

Hata hivyo ameongeza kuwa, hali hiyo imekuwa ikiwachanganya Wananchi na kuongeza gharama kwa Serikali kwani silaha zinakuwa zinamilikiwa na watu wengi lakini watu wasiwe na wasiwasi kuhusu maliasili na misitu, kuna wanaopambana na Majangili wataendelea kuwa na unifomu na silaha kwa kadri ya uzito wa majukumu.

Rais Dkt. Samia awaachilia huru wafungwa 2,240
Dola Milioni 25 zatolewa kumsomesha kila Binti