Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Dkt Noele Lwoga amewahasa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kujiunga katika umoja wa Makumbusho ya Taifa na Vyuo Vikuu ili waweze kupata fursa ya kujifunza kwa matendo na namna ya uhifadhi nakuendeleza urithi wa kitamaduni na wa asili.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa umoja ujulikanao kama Museum University Hub ulifanyika makumbusho na nyumba ya utamaduni.

“Hii Hub tuliyoizindua leo imeanzia Chuo Kikuu cha Dar es Salaaam, ni matarajio yetu vyuo vikuu vingine vinavyofundisha masomo ya urithi, Akiolojia, Historia na Utalii vitajiunga ili kutoa fursa kwa wanafunzi katika vyuo hivyo kukutana na wataalam wa Makumbusho ya TAifa ili waweze kushiriki shughuli za uhifadhi na kuendeleza mali kale” Amesema Dkt Lwoga.

Kwa upande wake Mkufunzi Mwandamazi katika fani ya Akioloji Chuo Kikiuu cha Dar es Salaam Dkt Egidius Ichumbaki ameipongeza makumbusho ya Taifa kwa kuanzisha mashirikiano hayo itawapatia wigo mpana wanavyuo.

Magufuli: Jengeni viwanda
DC mpya Ilala aapishwa