Mamlaka ya usimamizi wa shule nchini India umewataka Chuo cha The Bhagat kandika barua ya maelezo na kuomba msamaha kufuatia tukio lao la majaribio walilolifanya kwa wanafunzi kuwavalisha mabox kichwani kwa lengo la kutaka kukomesha tabia ya wanafunzi kupigiana chabo wakati wa kufanya mitihani yao.

Taarifa za chuo hicho kufanya tukio hilo, zilisambaa baada ya kupostiwa katika mtandao wa kijamii wa Facebook na mmoja wa wafanyakazi katika chuo hicho ambazo zilionesha wanafunzi wamevaa maboksi, huku sehemu ya mbele la maboksi hayo ikiwa wazi.

Msamamizi mkuu wa chuo hicho, MB Satish, amesema walitumia njia hiyo kukabiliana na udanganyifu wa kupiga chabo kwa wanafunzi na walifanya hivyo kama jaribio la muda tu kisha waliwatoa maboksi hayo kichwani.

“Hakuna mwanafunzi aliyelazimishwa kuvalia boksi kichwani. Kama unavyoona katika picha hizi kuna baadhi ya wanafunzi ambao hawajayaavaa, waliokuwa wameyavaa waliyavua baada ya dakika 15, wengine baada ya dakika 20 na hata sisi wenyewe tuliwaambia wayavue baada ya saa moja,” amesema MB Satish.

Ambapo katika ufafanuzi wao wameeleza kuwa kati ya wanafunzi 72 ni wanafunzi 56 tu ndio walikubali kuvaa maboxi kama sehemu ya jaribio hilo.

wanajisikia vizuri na jaribio hilo na chuo hakijamsumbua mwanafunzi yeyote kuhusu suala la kuvaa maboksi hayo,” amesema MB Satish.

Wakatoliki waandamana DRC kupinga ufisadi uliokithiri
Kibatari chateketeza nyumba na kuua watoto wawili