Wanafunzi 15 wa mafunzo ya kijeshi wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa mara baada ya kambi ya jeshi mjini Kabul nchini Afganistan kulipuliwa na mtu mmoja aliyejitoa mhanga.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afganistan imesema kuwa shambulio hilo limetokea siku moja baada ya mfuasi mmoja wa kundi la Islamic State-IS kushambulia msikiti uliojaa waislam wa dhehebu la kishia katika mji huo na kuuwa waumini 50 huku wengine wakijeruhiwa vibaya.

Polisi nchini humo na baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa shambulio hilo lililotokea mara baada ya mtu mmoja aliyekuwa akitembea kwa miguu karibu na basi hilo lililokuwa limejaa wanafunzi.

Wanafunzi hao walikuwa ndani ya basi hilo wakielekea katika shule ya kutoa mafunzo ya kijeshi ya Marshal Fahim iliyopo katika kambi ya jeshi hilo, huku msemaji wa wizara ya ulinzi ,Dawlat akithibibitisha kutokea kwa vifo hivyo.

 

Lukuvi kupambana na watakaoshindwa kuwajibika
‘Produza’ ajibu tuhuma za kumnyanyasa Lupita Kingono