Wanafunzi 195 wa kidato cha nne na darasa la saba wamepata mimba wakati wakiwa shuleni mkoani Simiyu hatua ambayo imesababisha kukatiza masomo yao.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Itilima, Bensoni Kilangi wakati akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka katika maadhimisho ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika mkoani humo.
Amesema kuwa katika mkoa huo, ameitaja wilaya ya Maswa ndiyo imekuwa na tatizo kubwa la wanafunzi kupata mimba.
Aidha, amesema kuwa serikali ya wilaya hiyo imeendelea kuwachukulia hatua kali wale wote ambao wamekuwa wakiwapatia ujauzito wanafunzi hao, ikiwamo kuwafikisha mahakamani.
“Mpaka kufikia mwaka 2016/17 watoto 195 kati yao 25 wa Shule ya Msingi na Sekondari 170 ndani ya mkoa wetu, tatizo hili hatutalifumbia macho wala kumlea mtu yeyote atakaye mpa mimba mwanafunzi,”amesema Kilangi
Kwa upande wake mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali la World Vision, Ngasa Michael amesema kuwa shirika hilo linaungana na Serikali katika vita dhidi ya Mimba.
Hata hivyo, baadhi ya Wanafunzi wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali wale wote wanaowarubuni wanafunzi wa kike.
-
TRA yataifisha mali za thamani ya shil. mil 3
-
Sheria mpya ‘kuwafunga’ wasiowatunza wazazi wao
-
Video: Mbowe ataja vipaumbele vitano bajeti ya upinzani, Masheikh na Maimamu waja na waraka mzito