Halmashauri ya Wilaya ya Wangingo’mbe mkoani Njombe inakabiliwa na idadi kubwa ya watoto ambao hawajaripoti shule za sekondari kuanza kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 licha ya shule kufunguliwa rasmi tangu january 8 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Wangingo’mbe, Ally Kasinge alipokuwa akizungumza na wananchi wakati akizindua Wodi ya wazazi katika kituo cha afya cha Kidugala kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzani, ambapo amesema kuwa wanafunzi 397 ambao walitakiwa kujiunga na kitado cha kwanza katika shule mbalimbali wilayani humo kwa mwaka wa masomo 2019 hawajaanza masomo.
Aidha, Kasinge amewataka wazazi na walezi kuhakikisha wanawapeleka wanafunzi hao shuleni kabla ya wiki moja na kwamba baada ya hapo serikali itawachukulia hatua za kisheria wazazi ambao wamekaidi kuwapeleka shule watoto na serikali itawafikisha mahakamani .
Kasinge pia ameliomba kanisa la KKKT kuwahamasisha waumini kupitia makanisa juu ya umuhimu wa kuwapeleka watoto hao shule kwa wakati ambapo Askofu wa KKKT Dayosisi ya kusini, Isaya Japhet Mengere amesema watashirikiana na afisa elimu wa wilaya hiyo ili kupata majina ya watoto hao na kushauriana na wazazi na kujua wamekwama wapi,
Hata hivyo, Mwitikio wa wazazi kupeleka watoto shule hususani kidato cha kwanza mkoani Njombe umekuwa mdogo kutokana na wazazi kuto ona umuhimu wa elimu na kusubiri kusukumwa na serikali.