Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kagera, inawashikilia wanafunzi 38 wa chuo cha ufundi (VETA), Kagera na wakufunzi wao wawili, Francis Mwangosi na Ssenabulya Daudi pamoja na Mkuu wa chuo hicho, Baluhi Mitinje kwa madai ya kukutwa na simu katika chumba cha mtihani.

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Taasisi hiyo Mkoani Kagera John Joseph imebainisha kuwa, TAKUKURU mkoani humo inawashikilia wanafunzi 21 wa Chuo cha ufundi Tuinuane na wakufunzi wao wawili, Charles Byabachwezi na Verdiana Myaka pamoja na mkuu wa chuo hicho Emmanuel Jonas kwa tuhuma za kufanya udanganyifu katika mitihani na matumizi mabaya ya ofisi kinyume na sheria.

Sambamba na hilo TAKUKURU imekamata simu 38 zilizotumiwa na wanafunzi ndani ya vyumba vya mitihani wiki iliyopita pamoja na shilingi 151,000/= zilizochanganywa na wanafunzi kwenye mchakato huo wa kuwapata wasimizi wa mitihani wa taifa wa elimu ya ufundi.

TAKUKURU imesema inaendelea na uchunguzi zaidi kabla ya hatua zaidi za kisheria kuchukuliwa dhidi ya wahusika wa tuhuma hizo.

Uongozi Mwadui FC wakanusha tuhuma
Namungo FC kumtumia Shiza Kichuya