Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge jana Jumanne Januari 6 amesema wanafunzi waliofaulu kuingia kidato cha kwanza mwaka huu watasoma kwa zamu kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa katika mkoa huo.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maandalizi ya shule kwa ajili ya wanafunzi hao, Kunenge amesema wamefikia hatua,ili wengine wasibaki nyumbani na itakapofika Februari 28,2021 wataendelea na utaratibu wa kawaida.

Kunenge amebainisha kuwa Tayari uongozi wa Mkoa umeomba kibali wanafunzi wote kuanza kwenda shule japo kwa zamu kutokana na uhaba wa madarasa ambapo wataanza Januari 11, 2021.

“Ila itakapofika Februari 28 ambapo ni agizo la Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa kuwa madarasa yawe yamekamilika na wanafunzi awamu ya pili wawe wameingia darasani wataendelea na utaratibu wa kawaida wa kwenda wote asubuhi,” amesema Kunenge.

Majaliwa: Vijana mna fursa ya ajira Nyasa
RC Mongella amuweka rumande Mkurugenzi Sengerema