Wadau wa Uuguzi na Ukunga wamekutana na kupanga mikakati ya kupunguza vifo vitokananvyo na uzazi na watoto wachanga kwa kuhakikisha huduma zinakuwa bora, na kuweka mazingira wezeshi ya huduma za afya ya uzazi.

Mkurugenzi wa huduma na Ukunga na Uuguzi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ziada Sellah amesema katika kuboresha hilo wamewashirikisha walimu wa vyuo vya ukunga ili wafundishe somo la huduma kwa mteja ili kuwawezesha wanafunzi kutekeleza vyema majukumu yao wanapoingia kazini.

Amesema kuwa watawajengea uwezo wakunga, kwa kuwa asilimia 90 ya akina mama wote wanaojifungua wanahudumiwa na wakunga.

Kwa upande wake rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), Fedy Mwanga amesema chama hicho kimejizatiti kutoa elimu kwa wauguzi na wakunga nchini kuhusiana na huduma bora za uzazi kwa mama mjamzito kabla na baada ya kujifungua kwa lengo la kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 15, 2020
Mradi wa kufua umeme Rusumo kukamilika mwakani