Baadhi ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini wamelalamikia ukosefu wa mikopo inayotolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, huku wengine wakidai kutowekwa kwenye orodha ya wanatakaopata mikopo licha ya kuwa kwenye fani ambazo zilitajwa na serikali kuwa zitapewa kipaumbele.

Wakizungumza nje ya jengo la Bodi hiyo lililoko Sinza jijini Dar es Salaam, baadhi ya wanafunzi hao walieleza kushangazwa na mgawanyo wa mikopo hiyo, huku wale ambao hawachukui masomo yaliyotajwa kama yanayopewa kipaumbele wakilalamikia mgawanyo huo kwa madai kuwa unawanyima haki walioamua kuchukua utalaam mwingine.

“Wanasema wanawapa zaidi faculty za udaktari, Petrol na Uhandisi. Je, sisi tunaosomea hivi vingine sio wanafunzi? Kwahiyo tunafanya kazi bure kusoma? Alihoji mwanafunzi mmoja. “Serikali inatakiwa ijue kwamba sio kuyapa kipaumbele masomo hayo tu, hata sisi tunaochukua Uchumi tutakuja kukuza uchumi wa hii nchi,” aliongeza.

Wanafunzi wengine walilalamika kuwa ingawa masomo wanayochukua yamepewakipaumbele kikubwa, lakini hawakuwekwa kwenye orodha ya kupata asilimia yoyote.

“Tumeambiwa kwamba masomo yetu yamepewa kipaumbele, lakini mpaka sasa hivi hata hiyo asilimia 0 sijapata, nimepewa ‘not secured’.”

Hata hivyo, Bodi ya Mkopo ilitoa ufafanuzi wa suala hilo ambapo ilieleza kuwa kuanzia mwaka huu wa masomo 2015/2016, wanafunzi wataanza kulipwa kiasi cha shilingi 8500 kwa siku ambacho ni ongozeko la shilingi 1000 ukilinganisha na mwaka wa masomo uliopita.

Bodi hiyo iliwataka wanafunzi kupuuzia taarifa zilizosambaa kwenye mitandao kuwa mwaka huu hawatapata mikopo kabisa bali wawe watulivu wakisubiri magawiwo yao na kuendelea na masomo.

Imeelezwa kuwa Bodi imepata ongezeko la mikopo zaidi ya Bilioni 100 ingawa bado hawajapata fedha hizo kutoka serikalini.

Jeshi la Polisi Lajitoa Maandamano Ya Bila Kikomo Ya Chadema
Njia rahisi za Kumgeuza Rafiki kuwa ‘Mpenzi Wako’ wa Dhati