Katika hali isiyo ya kawaida, wanafunzi sita wa shule ya Sekondari Usevya iliyoko wilayani Mlele mkoani Katavi wamempiga na kumng’oa meno matano mwalimu wao aliyetajwa kwa jina la Makonda Ng’oka Membele wakimtuhumu kuwadhalilisha.

Wanafunzi hao walimshambulia mwalimu huyo ambaye ni Makamu Mkuu wa shule hiyo wakishinikiza asiwafundishe kwa madai kuwa amekuwa akiwalawiti baadhi ya wanafunzi wa kiume kama adhabu mbadala kwa makosa wanayokutwa nayo shuleni hapo.

Mwalimu huyo aliwahi kufikishwa mbele ya Mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa tuhuma za kuwalawiti baadhi ya wanafunzi wa kiume, akidaiwa kufanya kosa hilo kati ya Novemba mwaka jana na Aprili Mwaka huu.

Hata hivyo, Mahakama ilikosa uthibitisho wa kutosha kumtia hatiani mwalimu huyo, hivyo kuamuru aachiwe huru.

Mbali na makamu huyo wa shule, wanafunzi hao pia wanadaiwa kumpiga na kumsababishia majeraha, mwalimu Gabriel Kambona. Ingawa sababu ya kumpiga mwalimu Kambona haijulikana moja kwa moja, hakuhusishwa na tuhuma za ulawiti.

JPM amuapisha Dk. Dau kuwa Balozi wa Tanzania Malaysia
Kesi ya Lema: Mahakama yatoa neno zito Upande wa Serikali