Wanafunzi walionusurika na mauaji katika shule ya sekondari Marjory Stoneman Douglas huko Florida nchini Marekani wametangaza maandamano mjini Washington na miji mingine muhimu ya Marekani mwezi ujao.
Maandamano hayo yanalengo la kushinikiza hatua thabiti zichukuliwa ili kuzuia mauaji mengine kama hayo yasitokee nchini humo.
“tutaandamana pamoja kama wanafunzi ili kuwaaibisha wanasiasa ambao wamekuwa wakikubali kupokea fedha kutoka chama cha wamiliki na watengeneza bunduki nchini Marekani-NRA. Na tutataka maisha yetu yalindwe.”Cameroon Kasey alipokuwa akifanya mahojiano na kituo cha televisheni cha ABC
Aidha, Mwanafunzi mwingine, Emma Gonzalez ameiambia ABC kwamba Rais Trump, Seneta Marco Rubio wa jimbo la Florida na gavana wa jimbo lao Rick Scott wanaunga mkono NRA na kuongeza kuwa hawatakwenda katika kikao cha Rais Trump siku ya Jumatano.
-
Raia wa Urusi washitakiwa kwa kuchakachua ushindi wa Trump
-
Wolper: Tanzania jina la nchi yetu naona si tamu tena na limeanza kuwa chungu
-
Gari la msafara wa Rais Kabila lapata ajali, laua
Hata hivyo, Ikulu ya White House imetangaza kuwa, Rais Trump atakutana na wanafunzi pamoja na walimu wao katika kikao cha kusikiliza madai yao ingawa haikutoa maelezo zaidi juu ya kikao hicho.