Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Imesela, iliyopo Kata ya Imesela, Wilaya ya Shinyanga, wamekuwa wakipiga kelele shuleni bila sababu huku taarifa zilizopatikana shuleni hapo Jumatano hii zimesema kwamba, wanafunzi hao wamekuwa wakianguka na kupiga kelele, tangu Januari mwaka huu

Kutokana na hali hiyo, walimu wa shule hiyo wamekuwa wakitumia muda mwingi kuwatuliza na hivyo kupoteza muda wa kuingia madarasani. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo yenye wanafunzi 252, Seleman Kalavina, amethibitisha uwepo wa tukio hilo na kusema kuwa wanafunzi kila wanapoanguka, huwa wanapiga kelele na kutamka maneno yasiyoeleweka.

Amesema jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika ikiwemo kuwaita viongozi wa dini, lakini tatizo hilo bado halijatatuliwa.

”Hali hii inatutisha hata sisi walimu kwani hatufundishi kwa vile tunatumia muda mwingi kuzima mapepo. Umefika wakati walimu wanatamani kuhama katika shule hii.”amesema Mwalimu Kalavina.

Aidha, amesema kuwa hali hiyo huwakumba wanafunzi wa kike peke yao na mauzauza hayo huanza saa moja na nusu asubuhi mpaka muda wa masomo unapomalizika mchana.

Kwa upande wake, Mratibu wa Elimu, Kata ya Imesela, Julius Wamba, amesema mauzauza katika shule hiyo yameongezeka kuanzia Machi mwaka huu ambapo watoto huwa wanapiga kelele, na kuwataja baadhi ya watu ambao huwasababishia hali hiyo.

Hata hivyo, Wamba amesema kuwa pindi tu hali inapojitokeza huwa wanawaita masheikh na wachungaji kuwaombea watoto hao lakini wakiondoka tu hali hiyo hujirudia na wanafunzi kushindwa kusoma.

Erik Lamela Kusubiri 2017/18
Alex Iwobi Ang'ang'ana Na Arsene Wenger