Mahakama ya Kijeshi nchini Sudani Kusini imewahukumu wanajeshi 10 vifungo vya kati ya miaka saba na maisha kwa makosa ya mauaji na ubakaji.
Wanajeshi hao wamepewa vifungo hivyo baada ya kukutwa na hatia ya kufanya mauaji na ubakaji kwenye ghasia zilizotokana na shambulizi liliofanyika katika hoteli ya Terrain iliyoko mji mkuu wa Sudani Kusini, Juba mwaka 2016.
Aidha, shambulizi hilo lilifanyika wakati wa mapigano makubwa kati ya vikosi vya serikali na vikosi vya waasi, ambapo zaidi ya watu 70 wakiwemo walinda amani wawili wa Umoja wa Mataifa (UN) waliuawa.
Katika ghasia hizo, mwandishi wa habari, John Gatluak aliuawa, na wafanyakazi wa kutoa huduma za kibinadamu walibakwa.
Licha ya vifungo hivyo, Mahakama hiyo imeiamrisha serikali ya Sudani Kusini kuilipa familia ya Gatluak ng’ombe 51 pamoja na kumlipa kila muathiriwa wa ubakaji dola za kiimarekani 4,000 kama fidia.
-
Trump aagiza kukamatwa kwa Mwandishi anayekosoa Serikali yake
-
Video: DC Katambi amsweka ndani aliyetaka kuvuruga mkutano wake na wananchi
-
LIVE: Rais Magufuli akihutubia wananchi wilayani Serengeti mkoa wa Mara
Hata hivyo, Tukio hilo lilikuwa baya zaidi dhidi ya raia wa kigeni tangu Wanajeshi wa Sudan Kusini kutuhumiwa kuendesha uhalifu mara kadhaa tangu yazuke mapigano ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2013.