Mapigano makali yametokea nchini Somalia kati ya majeshi ya serikali ya nchi hiyo na Wanamgambo wa Al-Shabaab na kusababisha vifo vya watu 22, kwa mujibu wa maafisa wa nchi hiyo.
Mapigano hayo yaliyotokea Kusini Magharibi mwa Somalia yalianza baada ya wapiganaji wa Al-Shabaab wenye silaha nzito walivyokuwa wakijaribu kuteka kituo cha jeshi katika mkoa wa Bay.
Afisa wa serikali ya Somalia amesema kuwa wanajeshi hao walikuwa katika mapambano makali kwa zaidi ya masaa sita wakiwakabili wapiganaji wa Al-Shabaab waliokuwa wameshambulia kambi ya jeshi kutoka pande nne.
“Walitushambulia kutoka maeneo manne ili waweze kuteka kambi mnamo majira ya saa moja asubuhi saa za hapa Somalia, baada ya masaa matano ya mapambano tuliweza kuwazuia na kulazimisha kukimbia,” amesema Kanali Osman Nurow.
Aidha, Nurow amesema kuwa majeshi ya serikali yaliyotumwa kutoka mji wa karibu wa Baidoa ili kusaidia kituo hicho waliingia katika mapambano hayo mara moja, na kuweza kuwaua wapiganaji wasiopungua 14.
-
Polisi waua magaidi 40 waliopanga kulipua makanisa
-
Mwandishi nguli wa ‘Killing Me Softly’ afariki dunia
-
Magaidi wateka mji, wasali pamoja na raia
Hata hivyo, kiongozi wa mkoa aliyechaguliwa Abdiaziz Hassan Mohamed, pia anajulikana kama Lafta Gareen, amesema majeshi ya mkoa huo yalipoteza wanajeshi nane katika mapambano hayo.