Maafisa wa usalama katika mkoa wa Belgorod nchini Urusi unaopakana na Ukraine, wamesema eneo la karibu na mpaka limekabiliwa na mashambulizi mengi ya ndege zisizo na rubani.
Gavana wa mkoa huo wa Belgorod, Vyacheslav Gladkov amesema mashambulizi hayo yameharibu majengo ya utawala, makaazi ya watu na magari, na kuongeza kuwa idadi kubwa ya ndege zisizo na rubani, au droni zilizohusika imedunguliwa.
Katika eneo hilo la magharibi mwa Urusi, kumekuwepo na matukio ya hujuma kwa miezi kadhaa ambapo Moscow inadai mawakala wa Ukraine wamekuwa wakiyafanya mashambulizi hayo kwa kutumia maguruneti na mizinga.
Hata hivyo, ripoti ya Urusi imesema wawakilishi wa vikosi vya jeshi la Ukraine’ wamekuwa wakiendesha operesheni katika mkoa huo na jeshi la Urusi liliondoa hali ya dharura iliyokuwa imetangazwa katika eneo hilo na kumaliza operesheni ya kigaidi.