Wanajeshi 16 wa Jeshi la Kenya (KDF) wanadaiwa kupoteza maisha huku wengine wakijeruhiwa vibaya baada ya helikopta waliyokuwa wakisafiria kuanguka eneo la Ole Tepesi kaunti ya Kajiado kilomita zaidi ya 70 kutoka jijini Nairobi nchini Kenya.

Jeshi la ulinzi la Kenya (KDF), limethibitisha ajali hiyo likisema helikopta hiyo aina ya Mi 171e ilikuwa kwenye shughuli za mafunzo ilipoanguka wakati ikijaribu kutua.

Ajali hiyo ilitokea mapema leo asubuhi na punde shughuli za uokozi zilianza.

Tayari shughuli za uokozi wa abiria zimekamilika na majeruhi wamepelekwa katika hospitali ya jeshi jijini Nairobi wakiendelea na matibabu.

Jeshi hilo limeeleza kuwa linawasiliana na familia za marehemu kwa sasa ili kuwapa taarifa na kutoa salamu za rambirambi.

Aidha wachunguzi wa ajali za ndege wapo katika eneo hilo kwa ajili ya kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Mamlaka yakanusha Mwanamke kujifungua mapacha 10
UEFA Euro 2020: 16 Bora kuwa ya moto