Utawala wa kijeshi nchini Niger, kupitia Televisheni ya Taifa umetangaza Mawaziri 21 wanaounda Serikali mpya ya nchi hiyo.
Hatua hiyo, imetukia wakati Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Ukanda wa Afrika Magharibi – ECOWAS ikikutana kwa mkutano wa kilele wenye azma ya kufikia maakubaliano juu ya hatua za kuchukuliwa dhidi ya Niger.
Mkutano huo wa kilele wa Viongozi wakuu wa Jumuiya ya ECOWAS, unafanyika katika mji mkuu wa Nigeria Abuja na huenda ukatoa mwelekeo kuhusu mkwamo uliopo nchini Niger.
Hata hivyo, Viongozi hao pia wanatarajiwa kukubaliana kuhusu hatua zitakazofuata baada ya mapinduzi hayo ya kijeshina huenda zikajumuisha uingiliaji kati wa kijeshi, hatua ambayo itakuwa ni suluhisho la mwisho endapo njia zote zitashindikana.