Wanajeshi nchini Cameroon wamewaua watu wanane katika maandamano ya kudai uhuru wa eneo la watu wanaozungumza lugha ya Kiingereza nchini humo.

Meya wa mji wa Kumbo ameeleza kuwa watu watano kati ya hao ni wafungwa waliopigwa risasi baada ya gereza kuchomwa moto na waandamanaji.

Waandamanaji hao ambao wanadai kunyanyaswa na watu wa eneo linalozungumza lugha ya Kifaransa, walitaka wafungwa wote wanaoshikiliwa kutokana na kushiriki maandamano ya kupinga unyanyasaji na kudai uhuru wao waachiwe huru.

Cameroon ilitawaliwa na wakoloni wa Uingereza na Ufaransa ambao waliacha matabaka ya wanaozungumza Kiingereza na wanaozungumza Kifaransa, baada ya Vita ya Kwanza ya Dunia.

Ingawa nchi hiyo iliunganishwa mwaka 1961, watu wanaozungumza Kiingereza wamekuwa wakilalamika kuwa wananyanyaswa na watu wanaotumia lugha ya Kifaransa ambao ni wengi zaidi.

Nedy Music afunguka alichokipata kwa Ommy Dimpoz
Video: Lema, Nassari wabonyeza kitufe, Mwinyi ataka Mawaziri wasijiuzulu