Wanamgambo 19 wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab wameripotiwa kuangamizwa kwenye operesheni iliyoendeshwa nchini Somalia.

Vikosi vya jeshi la Somalia vimetoa taarifa ya kuangamizwa kwa wanamgambo hao wa Al-Shabaab kwenye operesheni iliyoendeshwa eneo la Dinsoor mkoani Bay.

Akizungumza na kituo cha redio cha Jeshi la Somalia, Mkuu wa Jeshi la Somalia Jenerali Odowa Yusuf Rage, amebainisha kuwa walifanikiwa kuharibu kambi moja waliyokuwa wamekusanyika wanamgambo wa kigaidi.

Jenerali Odowa pia ameongeza kuwa operesheni hiyo iliendeshwa katika eneo la umbali wa takriban kilomita 11 kutoka Dinosoor kufuatia taarifa ya upelelezi iliyopokewa.

Katika wiki za hivi karibuni, jeshi la Somalia limekuwa likiendesha operesheni dhidi ya Al-Shabaab, operesheni zaidi zikiwa zimeendeshwa katika maeneo ya Kusini mwa nchi.

RC Dar awataka wananchi kulinda amani kipindi cha uchaguzi
NEC yaongeza muda wa kuapisha mawakala