Kituo cha jeshi la Marekani barani Afrika kimesema kuwa kwa ushirikiano na serikali ya Somalia jeshi la Marekani limefanya mashambulizi matatu ya angani nchini Somalia dhidi ya kundi la al-Shabaab ambapo wanamgambo 6 wameuawa.
Taarifa kutoka katika jeshi hilo la Marekani zinasema kuwa mashambulizi hayo yamefanyika kusini mwa Somalia umbali wa karibu kilomita 260 kusini mwa mji mkuu Mogadishu.
Al-Shabaab wametangaza kushirikiana na kundi la kigaidi la al-Qaeda na wameahidi kutoa mazingira ya kushirikiana katika mashambulizi ya kigaidi kote duniani.
Kundi hilo la al-shabab limetangaza wazi kujitolea katika kupanga na kuendesha mashambulizi dhidi ya Marekani na washirika wake eneo hilo.
-
Marekani itajuta kama itaendelea kutuchokoza: Korea Kaskazini
-
Jeshi la polisi Mtwara labaini mtandao wizi wa mafuta na vifaa vya ujenzi
Jeshi la Marekani linasema kuwa liitaendelea kutumia kila mbinu kuwalinda raia wake kutokana na vitisho kutoka kwa magaidi kwa lengo na kuwashambulia magaidi na kambi zao za mafunzo kote nchini Somalia na kote duniani.
Wakati huohuo polisi nchini Kenya wamewakamata watu wanne wanaoaminika kuwa raia wa Burundi ambao walikuwa wakielekea Somalia kujiunga na kundi la al-Shabaab.
Maafisa katika Ubalozi wa Burundi mjini Nairoibi wanasema kuwa watatoa taarifa kamili kuhusu kukamatwa huko baada ya kushauriana na mamlaka ya Kenya.