Kikosi Maalum cha Wanamgambo nchini Sudan cha RSF, kimesema kimechukua udhibiti kamili wa Ikulu ya rais, makazi ya mkuu wa jeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Khartoum.

Katika taarifa yake iliyotolewa hii leo Aprili 15, 2023 RSF imesema imechukua pia udhibiti wa viwanja vingine viwili vya ndege, kwenye mji wa kaskazini wa Merowe na mji wa El-Obeid ulioko upande wa kusini mwa nchi.

Kikosi hicho cha RSF kinachoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dagalo, maarufu kama Hemedti, kilisema jeshi lilizingira moja ya kambi zake na kufyatua risasi kwa kutumia silaha za kivita huku
vyama vya kiraia vya Sudan vikitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano yaliyozuka baina ya vikosi hivyo viwili.

Vyama hivyo ambavyo vimesaini makubaliano ya awali ya kugawana madaraka na jeshi la nchi hiyo pamoja na kikosi cha RSF pia vimetoa wito kwa wadau wa kimataifa na kikanda kuchukua hatua haraka kuzuia umwagaji damu.

Zijue harakati za kutafuta sheria bora ya Habari
Mohammed Ouattara aondoka kambini SImba SC