Andiko lililopita tumeona aina za wanawake ambao wanaume wengi huchukizwa nao, basi hapa leo tuangalie tabia za wanawake ambazo mara nyingi humvutia mwanaumme hata kufikiria kuoa au kuchukua uamuzi wa kuoa kabisa.
Yapo mahusiano ambayo yamedumu kwa miaka mingi lakini katika kipindi hiko chote mwanaume hajawahi kumtamkia mpenzi wake suala la ndoa, zipo sababu nyingi ambazo mwanamke anapaswa kujiuliza juu ya penzi la aina hiyo.
Je ni kweli mwanaume huyo bado hajamjua tabia yake au bado anatafakari zaidi juu yake.
Sasa hapa chini tumeangazia tabia ambazo mara nyingi wanaume huvutiwa nazo kutoka kwa wanawake.
Wenye msimamo
Wanawake daraja la kwanza wanaopendwa zaidi na wanaume ni wale wenye msimamo, uelewa mkubwa wa mambo na maamuzi sahihi, wako makini kwenye matendo yao na siku zote hufanya vitu kwa ajili ya kupata mafanikio.
Wapenda usawa
Aina ya pili inayohitajika katika katika ulimwengu wa kimapenzi ni wanawake wanaoheshimu usawa wa jinsia, walio tayari kubeba majukumu ya kifamilia kwa ulinganifu sawa na wanaume, wenye uwezo wa kuongoza jamii kwa asilimia 50 kwa 50.
Wenye urafiki ndani yake
Wanawake wenye sifa sawa na rafiki ni aina ya nne inayowavutia wanaume. Wao hutegemea zaidi nguvu ya kushawishi inayotokana na namna wanavyojali na kujitolea kuhakikisha wanakuwa marafiki wa kweli kwenye shida na raha kwa wapenzi wao. Si wakorofi, waungwana na wapenda amani.
Wanaojitegemea
Wanawake wanaojitegemea wana soko kubwa kwa wanaume tofauti na akina naomba vocha kila siku. Uchunguzi unaonyesha kuwa wanaume wa leo hawapendi wanawake tegemezi, wasiokuwa na kazi na wanaoendekeza starehe za upande mmoja.
Wanaoridhika
Wanawake ambao hulidhika na hali walizonazo ni kivutio kikubwa kwa wanaume, hili ni kundi linalohitajika sana katika ulimwengu wa mapenzi kwa upande wa wanaume ambao maisha ya sasa yamekuwa yakiwageuza kutoka juu kwenda chini au chini juu. Kukubali hali zote bila kubadili tabia ni sifa njema ya mwanamke.