Kikundi  cha Ibhasa Festival 2020 kimechanga zaidi ya Sh. milioni 3 kwa ajili ya kuwakatia Bima ya Afya wananchi 662 wanaotoka kwenye mazingira magumu katika Halmashauri ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.

Akizungumza na wanahabari, Makamu Mwenyekiti wa Ibhasa Festival 2020, Edo Mwamalala amesema kikundi hicho ambacho kinawakutanisha pamoja wazawa wa Kyela kutoka maeneo mbalimbali kimekuwa na mchango mkubwa katika kuisaidia jamii ya Kyela katika sekta ya afya na elimu kwa miaka miwili mfululizo.

Wananchi hao wamekatiwa Bima ya Afya iliyoboreshwa (CHF) ili waweze kupata huduma za afya bure kuanzia kwenye zahanati, vituo vya afya vya wilaya hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya.

Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Ibhasa Festival 2020, Nicolaus Mwangomo amesema moja ya mikakati ya Ibhasa ni kuboresha zaidi sekta ya Afya na Elimu kwa kuhakikisha wanayafikia maeneo yote ya Kyela ambayo yanauhitaji na kuwaomba wadau wengine kuchangia mpango wa CHF ili kuwahakikisha wananchi upatikanaji wa huduma ya Afya.

Mwangomo ameiomba Serikali kuboresha mazingira mazuri ya kutolea huduma kupitia dirisha la CHF kamainavyofanya kwa makundi mengine ya bima ya Afya.

Kaze arudisha 'KOMBORA' Tanzania Prisons
Tanzania Prisons waapa kuifunga Young Africans

Comments

comments