Serikali imeidhinisha fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo, zikiwemo shilingi 169 bilioni za kujenga mradi wa maji wa Nyangao-Ruangwa ambao utanufaisha wananchi katika vijiji 34 vya Ruangwa na 12 vya Nachingwea.

Hayo yamebainishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akizungumza na wananchi katika vijiji vya Mbecha, Nangumbu, Chimbila na Michenga akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo Wilayani Ruangwa, Lindi.

Amesema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kupunguza tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi waishio katika vijiji hivyo pamoja na vijiji vyote ambavyo mradi huo utapita, amewaomba wananchi hao waendelee kuwa na subira na imani na Serikali yao.

Naye, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel amesema Serikali imefanya maboresho katika hospitali ya Mkoa wa Lindi kwa kufunga mashine ya CT Scan, iliyogharimu kiasi cha shilingi bilioni mbili, hivyo imewapunguzia wananchi safari ya kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kufuata kipimo hicho.

Amesema, mbali na maboresho hayo pia Hospitali ya Kanda ya Kusini iliyoko mkoani Mtwara nayo imeanza kutoa huduma kwa wananchi. “Badala ya wananchi kwenda kufuata huduma za rufaa Muhimbili huduma hizo watazipata Mtwara.

Elimu Afya ya akili nguzo udhibiti matukio ya mauaji - Mlimba
OSHA yatoa uelewa utekelezaji wa majukumu yake