Wananchi wa Rwanda wamepewa nafasi ya kuipigia kura katiba mpya iliyoandaliwa inayomruhusu rais Paul Kagame kugombea urais kwa muhula wa tatu.

Baraza la Mawaziri la nchi hiyo limeidhinisha kufanyika kwa kura hiyo ya maamuzi ili kupata majibu kuhusu vuguvugu la kuongezwa kwa mihula ya rais Kagame kwakuwa katiba ya awali ilikuwa ikiweka ukomo wa mihula miwili tu anayoimalizia Kagame.

Baraza hilo la Mawaziri limetangaza kuwa kura hiyo kuhusu katiba mpya itafanyika Disemba 18 mwaka huu kwa wananchi wa Rwanda na Disemba 17 kwa raia wa Rwanda wanaoishi ughaibuni.

Uamuzi huyo wa Baraza la Mawaziri umeithinisha pendekezo la chama tawala cha nchi hiyo cha RFP iliyolitoa mwishoni mwa wiki iliyopita.

Katiba hiyo mpya inampa nafasi rais Kagame kugombea muhula wa tatu wenye muda wa miaka 7 huku ukimruhusu kugombea tena mihula miwili baadaye yenye miaka mitano kila mmoja.

Msichana aliyechukuliwa na Justin Bieber ageuka Mwehu, Polisi watinga hotelini
Picha: Profesa Jay Aanza na ‘Kazi Tu’