Wananchi wa Vijiji vya Mundindi katika Kata ya Mundindi na kijiji cha Ilininda katika Kata ya Madilu wilayani Ludewa mkoa wa Njombe wamejitokeza kwa wingi kuchimba barabara kwa kutumia zana za mikono zoezi lililofanyika kwa mtindo wa harambee.

Wananchi wa Kata hizo mbili za Mundindi na Madilu wamefanikiwa kuchimba Barabara inayotokea kijiji cha Mundindi kuunganisha na kijiji cha Ilininda ambapo zoezi hilo limeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Edward Haule ambaye amekuwa akishiriki uanzishwaji wa barabara mbalimbali katika maeneo tofauti ya vijiji vya Ludewa.

Aidha, akizungumza baada ya zoezi hilo, mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa Edward Haule amewahakikishia wananchi hao kuwa Halmashauri inatambua jitihada na juhudi za Wananchi hao walioamua kuanzisha barabara kwa mikono yao hatua itakayofuata kwasasa ni kuingiza barabara hiyo katika mfumo rasmi wa halmashauri ili iweze kutambulika na Wakala wa Barabara za Mjini na vijijini TARURA ili chombo hicho kiweze kuiendeleza.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kijiji cha Mundindi akiwemo, Ignasi Mgina (Mr.Katoto) wamesema kuwa barabara hiyo ikikamilika itakuwa msaada kwao kiuchumi hasa katika usafirishaji wa mazao kupitia kijiji cha Lusitu barabara ambayo inatajwa kuwa na mzunguko mfupi zaidi kuliko wanayoitumia sasa ambayo mzunguko wake ni mrefu hadi katika kijiji cha Mkiu.

 

Ndege aina ya Boeing 707 yaanguka na kuua 15
Mahakama yapiga chini shauri la kupinga Muswada wa Vyama vya Siasa