Wananchi Wilayani Makete mkoani Njombe wametakiwa kuendelea kutunza mazingira kwa kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji pamoja na kulima kilimo mbadala ili kuepuka utoroshwaji wa moto unaotajwa kuharibu mazingira kwa kiasi kikubwa.

Wito huo umetolewa na Afisa Mazingira halmashauri ya wilaya ya Makete mkoani Njombe, Upendo Mgaya wakati akizungumza na viongozi mbalimbali wa vijiji na vitongoji wa Kata ya Tandala wilaya ya Makete katika kikao cha kuhimiza utunzaji wa mazingira katika maeneo yao.

“Tunaagizwa tuhakikishe tunavilinda na kuvitunza vyanzo vya maji ili tuendelee kuyapata maji ya kutosha yatusaidie katika uhai wetu,”amesema Mgaya

Aidha, amewataka viongozi kutoa elimu kwa wananchi juu ya ukomo wa matumizi ya mifuko ya plastiki maarufu kama rambo ifikapo Juni mosi mwaka huu na kwamba baada ya muda huo kupita sheria zitaanza kuchukuliwa kwa watakao uza, kutengeneza pamoja na kutumia mifuko hiyo.

“Naamini mmesikia katika vyombo vya habari juu ya katazo la kutumia mifuko ya Rambo kwa hiyo tumeagizwa inapofika tarehe moja ya mwezi wa sita mwaka huu asionekane mtu anazalisha,anauza au anatumia mfuko wa Rambo kwa hiyo niombe kama viongozi kuanzia vitongoji, Kijiji mpaka Kata tukazidi kuhabarisha wananchi ili wapate uelewa,”ameongeza Mgaya.

Licha ya msisitizo wa kutofanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo vya maji lakini bado jamii wilayani humo inaamini nafasi ya kuruhusiwa kuendelea na shughuli hata kwa mita 30 kutoka katika chanzo kutokana jiografia ya wilaya ya Makete.

LIVE: YANAYOJIRI BUNGENI DODOMA LEO MEI 17, 2019
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 17, 2019