Wakazi wa Kata ya Makowo na vijiji vyake katika Halmashauri ya Mji wa Njombe Mkoani Njombe wameanza ujenzi wa kituo cha afya ili kuondokana na adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma za matibabu katika hospitali za mjini hali iliyokuwa inapelekea wanawake kujifungulia nyumbani.
Wakazi hao wamesema kuwa ukosefu wa kituo cha afya ambacho kingeweza kuwa na dawa za kutosha pamoja na huduma za upasuaji kwa wajawazito kumesababisha baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha.
Akizungumza na waandishi wa habari, Agnes Msemwa alisema ujenzi wa kituo hicho cha afya utawasaidia wakina mama ambao wamekuwa wakikutana na adha kubwa pindi wakitaka kujifungua kwani kutokana na ukosefu wa kituo cha afya wanawake wengine wamekuwa wakijifungulia nyumbani.
‘’Sisi akinamama tulikua tunapata shida ambayo ilikuwa inapelekea kujifungua nyumbani na mara nyingine wengine walikuwa hawafiki katika kituo cha afya wanakuwa wameshakufa kutokana na umbali mrefu’’amesema Agnes.
Naye Basil kasuva amesema kuwa kukosekana kwa kituo cha afya katika maeneo yao ilikuwa ni changamoto kutokakana na huduma hiyo kupatikana umbali mrefu.
‘’Tumeamua kujenga kituo hiki cha afya kwa nguvu zetu ili kuweza kupata huduma kwa wakati sahihi…kwani mpaka ufike mjini ni zaidi ya kilometa 100’’alisema Kasuva.
-
10 Watiwa mbaroni kwa kuhamasisha maandamano
-
DC Kasesela awafunda wasanii wa filamu nchini
-
Alichokisema Goodluck Gozbert baada ya kukutana na JPM
Kwa upande wa diwani wa kata ya makowo honoratus mgaya alisema kituo hicho kikikamilika kinatarajia kuhudumia wakazi wa kata tatu ambako wanakabiliwa na ukosefu wa kituo cha afya.
Kwa upande wake, Mkurungenzi wa halmashauri ya Mji wa Njombe, Illuminata Mwenda amesema kuwa wameunga mkono jitihada za wananchi hao kwa kutoa fedha za kumalizia mradi huo.