Wakazi wa Kijiji cha Nandete wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara wamejiwekea utaratibu wa kuchangishana kwa hali na mali pamoja na kujitolea nguvu kazi kukamilisha ujenzi wa Jengo Jipya la Zahanati, baada ya kuona Zahanati iliyopo inaelemewa na kushindwa kutoa huduma ipasavyo kwakua inategemewa na wananchi kutoka vijiji vitano.
Wakizungumza na Dar24 Media wilayani humo, Wananchi hao wamesema kuwa jengo lililopo ni dogo na linasababisha baadhi ya huduma kushindwa kutolewa ipasavyo licha ya Dawa na vifaa tiba vyote muhimu kuwepo hatua iliyo wasukuma kuanza ujenzi wa jengo hilo jipya.
“Ukiangalia Zahanati yetu hakuna tatizo la Dawa, hapa Dawa zote muhimu zipo ila sasa Majengo ya zahanati ni madogo ukiangalia wanao tibiwa katika kituo hiki tupo wengi kutoka karibia vijiji vitano”.amesema mmoja wa wakazi wa kijiji hicho aliejitambulisha kwa jina la Fatuma Machiko.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Dkt. Furaha Mwakafwira amesema kuwa majengo ya Zahanati iliyopo katika kijiji hicho ni ya muda mrefu ambapo ilijengwa mwaka 1992 na sasa inahudumia wananchi wa vijiji vitano na kuna wastani wa wagonjwa 50 mpaka 60 kwa siku , hali ambayo inasababisha Jengo lililopo kuwa Dogo.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mtwara, Yusuph Nanila ambaye amefika katika Zahanati hiyo na kujionea jitihada zilizoonyeshwa na wananchi aliwataka viongozi wa serikali kuwaunga mkono wananchi hao waliojitolea kwa hali na mali kuanzisha mradi huo.
-
Waziri Mkuu atoa siku 21 kwa viwanda vyote vya vileo nchini
-
Spika azungumzia hatma ya sakata la CAG na Mdee
-
Milioni 451 kuboresha Elimu Wilayani Mtwara
Hata hivyo, Sera ya serikali ni kuendeleza miradi ya maendeleo iliyojiwekea kipaumbele na kuibuliwa na wananchi ambapo katika mradi huu wa Zahanati wito wa wananchi ni kuitaka serikali kuwaongezea nguvu na kuwaunga mkono kufanikisha kukamika kwa ujenzi huu.