Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetenga Tsh Bilioni 1.2 kwa ajili ya awamu ya kwanza ya mradi wa ujenzi wa nyumba za wananchi watakaokubali kwa hiari kuhama katika hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.
 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiongea na wananchi wa Ngorongoro

Waziri Mkuu ameyasema hayo, Machi 13, 2022 wakati akizungumza na wananchi katika kijiji cha Msomera kabla ya kukagua ujenzi wa nyumba hizo ambazo kati yake nyumba 53 zimepauliwa na hatua za umaliziaji zinaendelea, nyumba 42 zipo hatua ya boma na nyumba 8 zipo katika hatua za ujenzi wa msingi. 

Awamu hiyo ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huo inahusisha nyumba 103 ambazo zipo katika hatua mbalimbali.

Ujenzi wa nyumba hizo ulianza tarehe 28 Februari 2022 na hadi kufikia Machi 12, 2022 ujenzi huo umefikia asilimia 78.

Nyumba hizo zinajengwa katika kijiji cha Msomera Wilayani Handeni, mkoani Tanga.

RS Berkane wamshtaki Ndala CAF
Jinsi wanaume wanavyopata hedhi