Wananchi wa Kata ya Nkuyu wilayani Kyela Mkoani Mbeya wamesema kuwa wamejipanga kikamilifu kuboresha sekta ya kilimo kwa kuongeza uzalishaji wa zao la Kokoa ambalo ni kipaumbele cha uchumi kwa wananchi.

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Dar24 Media ambapo wamesema kuwa licha ya kuzalisha zao hilo baadhi yao bado hawana muamko wa kutosha kutokana na kujisahau na mazao ambayo hayana faida kwa mkulima.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Nkuyu, Kain Mwakanyemba amesema kuwa zao la Kokoa ni zao lenye faida kiuchumi kwa wakulima wa Nkuyu hivyo wanapaswa kulipa kipaumbele.

‘’Baadhi ya wakulima bado hawana mwamko juu ya zao hili kwakuwa wamejikita zaidi kuzalisha mazao mengine ikiwemo mpunga lakini tunaendelea kutoa elimu ili zao hili lipewe kipaumbele maana hata bei zake ni zaidi ya mpunga,” amesema Mwakanyemba

 

 

Wafanyabiashara soko kuu Mafinga wakarabati barabara za ndani ya soko kuondoa vumbi
Majaliwa awatangazia kiama wanaoteka watoto