Hali si shwari katika jimbo la Mtama ambapo wanachama wa CCM wameandamana kupinga ushindi wa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye katika kura za maoni.

Wananchi hao waliobeba mabango yenye jumbe mbalimbali wamendamana wakishinikiza chama hicho kutengua matokeo ya Nape huku wakimtaka mgombea aliyeshika nafasi ya pili katika kura hizo, Suleiman Mathew kukihama chama hicho endapo matokeo hayo hayatatenguliwa.

Katika matokeo yaliyotangazwa ya kura za maoni, Nape alipata kura 9,344 na Suleiman alimfuata kwa kupata kura 4,766. Hata hivyo, ilionekana kuwa idadi ya jumla ya kura zilizotangazwa inazidi idadi ya wapiga kura hali iliyozua wasiwasi wa kuwepo kwa goli la mkono.

Suleiman yupo katika jimbo hilo akifanya majadiliano na watu wake wa karibu kuhusu uamuzi anaopaswa kuchukua huku Kamati Kuu ya CCM iliyokaa mjini Dododoma ikitaja majimbo ambayo yatarudia upigaji kura lakini jimbo hilo halikutajwa.

Rafael: Van Gaal Hapedezwi Na Wachezaji Wa Brazil
Upepo Wa Usajili Wa Pedro Wabadili Muelekeo