Wananchi waliokumbwa na ‘bomoabomoa’ katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam wamevamia shamba la waziri mkuu wa zamani, Frederick Sumaye lenye ukubwa wa hekari 33 lililopo katika eneo la Mji mpya, Mabwepande na kujigawia maeneo.

Waandishi wa habari walishuhudia baadhi ya wananchi wakijigawia maeneo kwenye shamba hilo huku wengine wakijenga nyumba za miti na nyumba za matofari.

Sumaye amekiri kuvamiwa kwa shamba lake na wananchi hao zaidi ya 100 lakini amesema kuwa hana wasiwasi kwa kuwa eneo hilo analimiliki kihalali na ana hati inayompa haki ya umiliki kisheria.

Waziri Mkuu huyo wa zamani alieleza kuwa atafuata taratibu za kisheria na atarudishiwa shamba hilo. Alisema hatua za kurudishiwa kwa shamba lake zimeanza kufanywa na mamlaka husika na kwamba hatatumia nguvu katika kuwaondoa wananchi hao.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Mkaonda alikiri kupata taarifa kuhusu uvamizi wa eneo hilo lakini hajapata malalamiko rasmi kutoka kwa Sumaye.

“Hilo shamba linalodaiwa kuwa ni la Sumaye, sijawahi kupokea malalamiko kutoka kwake dhidi ya uvamizi huo ila niliwahi kupigiwa simu na mmoja wa Makamanda wa Polisi Mkoa ambaye alinieleza kuhusu uvamizi huo,” alisema Makonda.

Makonda alieleza kuwa mbali na shamba la Sumaye, alipata taarifa kuwa wananchi hao pia wamevamia shamba la aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu, Daudi Balali.

 

Mchungaji Lwakatare Aigomea Serikali Kuvunja Jumba Lake
Sikuelewi! Utajiri Huu wa Ridhiwani Ni wa Kutisha