Abel Paul, Jeshi la Polisi – Dar es Salaam

Jeshi la Polisi limewakumbusha wananchi kushiriki katika masuala ya kijamii ikiwa ni Pamoja na kuyakumbuka makundi maalum ya wahitaji yaliyopo katika jamii inayowazunguka, ili kujenga ustawi kwa watanzania.

Hayo yamebainishwa na Mrakibu Msaidizi wa Polisi, ASP Sinasubi Serungwi akiwa katika kituo cha Udiakonia cha kilutheri Mtoni Dayosisi ya Mashariki na Pwani, ambapo amesema jamii inapaswa kushiriki na kutoa mahitaji katika vituo na makundi ya wahitaji kama walivyo fanya wao Jeshi la Polisi.

Amesema, kituo hicho kinahitaji sana misaada mbalimbali ambapo amewaomba wananchi kufika na kuwafariji Watoto hao huku akibainisha kuwa wamefika katika kituo hicho ikiwa ni sehemu ya sala na majitoleo yao katika umoja wa madhehebu ya kikristo kutoka chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam – DPA.

Aidha, Mkaguzi wa Polisi Insp. Paul Bundala amewaomba wananchi kuendelea kushiriki na kufika katika vituo vya kulea watu wenye uhitaji na kutoa misaada kwa makundi hayo maalum katika jamii ili kufanya wajione kama makundi mengine katika jamii.

Kwa upande wake Mkuu wa kituo cha Udiakonia, Bi. Winfrida Malumbo amewashukuru maafisa wa Jeshi la Polisi kutoka chuop cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) kwa kuonyesha upendo kwa kituo hicho ambacho kinalea Watoto wenye uhitaji maalum.

Naye Mwanafunzi wa kozi ya uofisa Rebaca Mwakibibi ameushukuru uongozi wa chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam (DPA) kwa kuwapa kibari cha kushiriki na kutoa misaada yao katika kituo hicho ambacho huku akibainisha kuwa wao ni Polisi lakini bado ni sehemu ya Jamii na waliona vyema kufika nakutoa msaada wao alisema Mwakibibi.

Maadili: Jamii ishirikiane katika malezi ya watoto
TEHAMA waanzisha mradi kituo cha Taifa cha ubunifu