Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Ridhiwani Kikwete amewashukuru wananchi wa kata ya Ruaha , halmashauri ya Iringa kwa ubunifu wa miradi inayolenga kutatua kero za wananchi.
Ridhiwani ametoa shukurani hiso baada ya kutembelea nakuona jinsi Wananchi wa eneo hilo walivyojitoa na kuhakikisha wanamaliza kero mbalimbali kwa kushirikiana na Serikali ili kuharakisha shughuli za kimaendeleo.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha Naibu Waziri, Mbunge wa jimbo la Iringa, Jesca Msambatavangu ameishukuru Serikali kwa kutenga fedha Bilioni 51 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za TASAF na pia kuishukuru kwa kuleta pesa ndani ya muda.
Audha, Naibu Waziri pia aliwashukuru na kuwapongeza wananchi hao kwa ubunifu wao wa ujenzi wa kivuko ambacho sio tu kinakwenda kuunganisha mitaa mitatu katika mahitaji lakini kitasaidia watoto kwenda shule na wananchi kupata huduma muhimu hasa kipindi cha mvua.