Wananchi wa Kijiji cha Isimike Kata ya Saja wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe wamelazimika kujenga madarasa mawili na ofisi katika shule ya msingi Isimike ili kukabiliana na mlundikano wa wanafunzi katika madarasa yaliyopo.
Taarifa ya kijiji cha Isimike iliyosomwa na afisa mtendaji wa kijiji hicho, Julius Mpiluka mbele ya mbunge wa jimbo la Wanging’ombe Mhandisi, Gerson lwenge katika ziara yake ya kibunge imeeleza kuwa zaidi ya shilingi milioni 14 zimetumika hadi sasa katika ujenzi huo uliofikia usawa wa lenter.
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Isimike, Nichorus Kabelege amesema kuwa bado shule hiyo itaendelea kukabiliwa na upungufu wa madarasa saba katika shule hiyo baada ya kujengwa madarasa hayo mawili yanayokaribia kukamilika.
“Kwasasa baada ya kuongeza madarasa haya mawili tumekuwa na madarasa 8 kati ya 6 tuliyokuwa nayo, kwa hiyo tunaupungufu wa madarasa saba ambayo tunaendelea kuyajenga taratibu,kwa jengo hili ambalo linaendelea, tunaiomba serikali iendelea kutusaidia pamoja na kutumia nguvu ya wananchi, wahisani pamoja mheshimiwa mbunge lakini bado kunahitajika kukamilishwa kwa maana ya finishing kwa ujumla,”amesema Kabelege
Naye mbunge wa Jimbo hilo, Gerson lwenge ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa madarasa na ofisi hiyo huku akiwataka kukamilisha zoezi la upigaji mbao ili awapelekee bati zitakazotosha katika majengo hayo.
-
Bodi ya Mikopo yawageukia Wastaafu, ‘Lazima walipe deni’
-
SABASABA: PPRA yatoa elimu ya mfumo wa manunuzi kwa njia ya mtandao
-
Tanzania yazidi kupaa katika mapambano dhidi ya Rushwa
“Mmeniomba bati ya jengo hili,na mimi kwasababu nilitoa ahadi jengeni maboma,najua serikali itakuja kutupatia nguvu lakini wakati tunaisubiri serikali na mimi mbunge nitatoa hizo bati 150”amesema Lwenge