Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Benno Malisa ameweka jiwe la msingi katika kituo cha Afya ulenje kilichopo katika halmashauri ya mbeya vijijini ambapo kituo hicho kinaendelea kujengwa kwa nguvu za Wananchi ujenzi ambao uliaza Agosti 2022 na hadi sasa umefikia hatua ya renta huku wakiiomba Serikali kuwaunga mkono katika umaliziaji wa kituo hicho

Akitoa taarifa ya ujenzi huo wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi, Diwani wa Kata ya Ulenje Mhandisi Boniface Njombe amesema kwa kutambua umuhimu wa huduma za afya wananchi wake walianza ujenzi wa Kituo cha afya kwa kujenga majengo mbalimbali kuanzia Agosti 2022 ikiwemo kujenga jengo la mama na mtoto, jengo la upasuaji, mapokezi na jengo la wagonjwa wa nje na wamefikia hatua ya Renta na kuwashukuru wadau walioshirikiana nao pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Oran Njeza.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Benno Malisa.

Katika ujenzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amechangia Shilingi Million moja kwa wananchi wa Kata ya Ulenje kuwaunga mkono kwenye ujenzi huo, ili kusaidia kuboresha huduma za afya huku Mkuu huyo wa Wilaya kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Juma Homera akisema atahakikisha anafikisha kilio na ombi lao kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Naye Mbunge wa Mbeya vijijini, Oran Manasse Njeza amewapongeza wananchi wake wa Kata ya Ulenje kwa kuungana kujenga kituo cha afya na kuahidi kuendelea kuikumbusha Serikali kuwaunga mkono huku naye akichangia tena Shilingi milioni mbili.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera

Aidha, Malisa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera kwenye uwekaji huo wa jiwe la msingi, amesema atahakikisha anafikisha kilio na ombi la wana Ulenje kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan la kuungwa mkono kwenye umaliziaji wa ujenzi huo, unaohitaji fedha zaidi ya Sh. Million 400 ambapo Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ikiahidi kuchangia shilingi laki tano ili kuwaunga mkono wananchi.

Hata hivyo, Wananchi hao wa kata ya Ulenje wanasema wamekuwa wakihangaika kutafuta huduma za afya za uhakika maeneo ya mbali na hulazimika kujifungulia njiani hivyo kujengwa kwa kituo hicho kutakuwa mkombozi hasa katika huduma za uzazi na mtoto.

Banda, Onyango waivuruga Simba SC
PICHA: Fei Toto aanza mazoezi Azam FC