Wananchi wa Jimbo la Tanganyika wamepigwa na butwaa kumuona Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo – DRC, Felix Tshisekedi akinadi sera zake jimboni humo ikiwa ni mara ya kwanza kuingia eneo hilo tangu alipochaguliwa kuwa kiongozi wa nchi hiyo.

Rais Felix Tshisekedi akiwasili jioni jimboni humo ikiwa ni mara ya kwanza toka aingie madarakani kama Rais na safari hii alikuwa akiomba tena wamchague kupitia chama tawala cha UDPS, akiungwa mkono na Vyama vingine vidogo vya Union Sacré nchini humo.

Maelfu ya raia walimsubiri kwa hamu kiongozi huyo wa nchi, huku wakiwa na shauku ya kumuona kwa mara ya kwanza, wakitegemea kupata hotuba itakayosaidia kuboredha maisha yao katika Jimbo hilo la Tanganyika lenye usalama mdogo.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa wa DRC, Kalinde Bavon alisema kuwa ujio wa Rais Tshisekedi Wilayani Tanganyika, ulisaidia raia wa eneo hilo kujua maendeleo ya nchi yao endapo Kiongozi huyo atachaguliwa tena.

Familia zaelimishwa kinga magonjwa ya mlipuko Hanang'
Licha ya Mafuriko: Morogoro yapeleka msaada Hanang'