Kundi la wananchi katika eneo la Fela wilayani Misungwi mkoani Mwanza unapojengwa mradi wa Reli ya Kisasa (SGR), kati ya Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga, wamesimamisha msafara wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu huku wakitoa kilio cha kunyimwa ajira katika mradi huo.

Wananchi hao ambao wamekita kambi katika eneo hilo tangu mwaka 2021 wamezuia msafara huo leo Machi 14, 2022 na kusababisha wajumbe wa kamati hiyo kusimama kuwasikiliza kilio chao.

Mwenyekiti wa wananchi hao, Paulo Mnema amesema pamoja na wananchi hao kutoka maeneo tofauti nchini kukaa muda mrefu bila kupewa ajira katika mradi huo, bado kuna urasimu katika ajira zinazotolewa kwani baadhi yao wanaombwa rushwa ili kupatiwa ajira hizo.

Akizungumza baada ya kusikiliza kilio cha wananchi hao, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Seleman Kakoso ameahidi kufikisha kilio chao serikalini.

Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Veronica Kessy amekiri wananchi hao kutolipwa fidia huku akisema kinachokwamisha ni taratibu za malipo.

Reli hiyo yenye urefu wa kilometa 341 inaanzia Fela wilayani Misungwi mkoani Mwanza hadi Isaka mkoani Shinyanga inatarajia kugharimu zaidi ya Sh3 trilioni.

Waziri Mkuu Majaliwa awapa maagizo wakuu wa mikoa
Vyombo vya habari kukuza kiswahili