Wananchi wa Jiji la Dar es Salaam wamesogezewa huduma za kısasa za kinywa na meno kwa kuhusianisha na afya ya binadamu kwa ujumla.
Kituo hicho cha afya ambacho kitajihusisha zaidi na kuimarisha huduma za kinga ya meno imezinduliwa jijini Dar es Salaam ili kutoa suluhisho la kudumu la matatizo ya meno nchini.
Mtendaji Mkuuu wa Kliniki hiyo inayojulikana kama AFYA BORA COMPLETE DENTISTRY LTD, Dkt. Donna Williams Ngirwa amesema kituo hiki kitajikita zaidi katika kueneza elimu kuhusu uhusiano uliopo kati ya afya ya kinywa na afya ya binadamu kwa ujumla.
“Utafiti unaonyesha kuwa magonjwa mengi yakiwemo magonjwa ya kudumu kama shambulio la moyo, kisukari, kiharusi, maambukizi katika mapafu na magonjwa mengine yana mahusiano ya karibu na maambukizi yaliyopo kinywani,” amesema Dkt Ngirwa.
Pamoja na kutoa huduma ya meno kliniki hiyo imekuwa ikitoa mafunzo kuwawezesha madaktari bingwa wa meno hapa nchini kutoa huduma za kipekee za meno na wanatoa fursa kwa wahitimu wa elimu ya juu kikiwemo Chuo Kikuu cha Afya ya Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) ili kujifunza na kuimarisha fani ya udaktari wa meno.
Dkt. Ngirwa amesema mpango wa Afya Bora ya Meno utatoa huduma bure za uchunguzi wa meno, usafishaji wa meno, vipimo vya x-ray, na punguzo la asilimia 20 kwa tiba kamili ya meno.
Kwa mujibu wa Dkt. Gilbert Tarimo ambaye ndiye daktari bingwa katika kituo cha huduma ya meno na kinywa cha AfyaBora,amesema lengo ni kuifanya huduma ya afya ya kinywa kuwa ya kinga zaidi badala ya tiba.
“Tunafanya uchunguzi wa afya ya kinywa na mgonjwa anapewaripoti ya kila kitu kuhusu kinywa chake na hatua anazopaswakuchukua ili kuboresha afya yake zaidi,” anasema Dkt. Tarimo.
Kituo hicho kilichoko mtaa wa Regent Estate jijini Dar esSalaam kinatoa huduma zote za meno ikiwemo usafishaji wa meno, kuweka meno ya bandia, mpangilio wa meno na lengo kuu la Afya Bora ya Meno na Kinywa ni kuwajenga wananchi wawe na utamaduni wa kuthamini afya ya meno na kinywa ili kuboresha maisha yao.