Mkoa wa Pwani umepiga marufuku uingizwaji na uchinjaji wa Nguruwe mkoani humo ili kukabiliana na homa ya Nguruwe African Swine Fever unaodaiwa kuingia mkoani humo.
Hayo yamesemwa na Ofisa Habari wa Halmashauri ya Mji wa wa Kibaha, Innocent Byarugaba alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema kuwa ugonjwa huo uliingia mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu kwenye kata mbili za Picha ya Ndege na Viziwaziwa eneo la Mikongeni.
“Wananchi wawe na tahadhali ,ugonjwa huu tayari umesababisha vifo vya nguruwe 71 na baada ya kufanyiwa uchunguzi wa awali kupitia dalili za wanyama hao na kwa wale waliokufa viashiria vilionyesha ni ugonjwa huo,” amesema Byarugaba.
Hata hivyo, ameongeza kuwa nguruwe waliokufa walichukuliwa Sampuli na kupelekwa maabara kuu ya mifugo Temeke Jijini Dar es salaam na kubaini uwepo wa ugonjwa huo.