Afisa Tarafa ya Mlangali wilayani Ludewa mkoa wa Njombe, Ezekiel Magehema amewataka Wananchi wa Kijiji cha Ludende Kata ya Ludende Kutambua kazi na mchango mkubwa unaofanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli.
Ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Ludende wilayani Ludewa huku akiwapongeza wananchi hao kwa kazi ya ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika Kituo cha Afya cha Kata ya Ludende ambalo lipo katika hatua za mwisho.
“Wajasiriamali wadogo wadogo ambao hawana vitambulisho vya biashara viliyotolewa na Rais Magufuli naomba wahakikishe wanakuwa navyo ili kuepusha usumbufu wawapo kwenye biashara zao, hili litatufanya sisi tumuunge mkono Rais wetu kwa Vitendo,”amesema Magehema
Kwa upande wake, mwenyekiti wa kijiji hicho, Samwel Shagama amewataka wananchi hao kuendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali za kuwasogezea huduma za maendeleo wananchi.
-
Wananchi watakiwa kuunga mkono juhudi za Serikali.
-
TACIP yamkabidhi Pierre tiketi ya kwenda Misri Bungeni
-
Serikali kubuni njia mbadala ya kutibu ugonjwa wa Dengue