Maelfu ya wananchi wamekusanyika mjini Niamey nchini Niger kuunga mkono mapinduzi yaliyofanyika Niger mwezi uliopita pamoja na hatua ya kufukuzwa balozi wa Ufaransa.

Wanachi hao ambao wanauunga mkono utawala mpya wa kijeshi ulioingia madarakani baada ya kumpindua Rais wa nchi hiyo Mohamed Bazoum.

Raia hao wa Niger walikusanyika katika uwanja mkubwa zaidi nchini humo wa Seyni Kountche wenye viti 30,000, uliojaa kwa theluthi mbili, huku bendera za Niger, Algeria na Urusi zikitawala.

Hata hivyo, Wizara ya mambo ya kigeni ya Niger ilitangaza kumtimua balozi wa Ufaransa Sylvain Itte kwa madai kwamba alikataa kukutana na watawala wapya. Iliongeza kuwa vitendo vya serikali ya Ufaransa vinakinzana na maslahi ya Niger.

Ubora wa Chumvi: Waziri Mkuu atoa maagizo
Rais atangaza marufuku ya kutoka nje, Intaneti yazimwa