Wakazi wa Gairo mkoani Morogoro, wamevamia lori la mafuta lililopinduka na kukinga mafuta bila kujali hatari inayoweza kuwapata eneo la mpakani mwa mji huo wa Gairo na Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remedius Mwema Emmanuel amesema Mamlaka Wilayani humo, zimefanikiwa kuondoa umati wa wananchi uliokuwa umevamia lori hilo wakiwa wamebeba ndoo na vidumu walionekana kuzingira lori hilo.
“Nimefika eneo la tukio, awali ilisemekana ni Gairo lakini ni Kongwa. Tumefanikiwa kuwaondoa wananchi katika lori hilo na taratibu zingine za kiusalama zinaendelea,” amesema DC Mwema.
Miaka miwili iliyopita, ajali iliyohusisha gari la mafuta lilopinduka na kuwaka moto Mkoani morogoro ilisababisha vifo vya watu zaidi ya 100 na majeruhi kadhaa.